Kuuza
Hati (Ankara na Nukuu za Bei)
Ankara, nukuu za bei, risiti, delivery note na zaidi, zinazochapishwa kwa kiolezo chako mwenyewe.
Ilisasishwa 04 Nov 2026
Tengeneza hati
Hati → Hati Mpya: chagua aina (ankara, nukuu ya bei, proforma, risiti, delivery note ...), mteja, mistari na sehemu zozote za masharti. VAT na punguzo vinahesabiwa.
Malipo ya ankara
Fungua ankara na weka malipo (fedha taslimu, pesa za simu, benki). Hali yake inafuata: Haijalipwa, Imelipwa Sehemu, Imelipwa. Ankara zilizopita muda zinaonekana kwenye tahadhari za asubuhi.
Violezo na chapa yako
- Violezo: chagua mpangilio wa kila aina. Kila kiolezo kina picha (ibofye kuiona kubwa), na picha iliyo kando ya kila aina inafuata kiolezo unachochagua.
- Picha na Taarifa: nembo, muhuri, sahihi, taarifa za benki na alama ya maji (watermark).
Muhuri na sahihi
Kwenye kila hati, chini ya Show on the Document (onyesha kwenye hati), Stamp (muhuri), Signature (sahihi) na Signature line and who signs (mstari wa sahihi na anayesaini) ni visanduku vitatu tofauti. Kutuma nakala laini (soft copy) moja kwa moja kwa mteja ikiwa na muhuri tu, acha tiki kwenye Stamp na ondoa tiki kwenye vingine viwili.
Nakili na geuza
Geuza nukuu ya bei kuwa ankara, au nakili hati.
Ankara na nukuu za bei za miradi kutoka BOQ pia zinatengenezwa hapa (ona Kutoza Miradi).
